2 Chronicles 8:1-6

Shughuli Nyingine Za Sulemani

(1 Wafalme 9:10-28)

1 aMiaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alilijenga Hekalu la Bwana na jumba lake mwenyewe la kifalme, 2Sulemani akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo. 3 bKisha Sulemani akaenda Hamath-Soba na kuuteka. 4 cPia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi. 5 dAkajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo. 6 eSulemani pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.

Copyright information for SwhKC